
Ligi Moja, Upendo Mmoja, Vumbi Moja
Msimu wa 2026
Pande Cup 2026
Karibu kwenye Pande Cup 2026 - mashindano ya soka la mchangani yanayoleta pamoja ushindani, jamii na teknolojia katika mfumo mmoja wa kidijitali. Kabla ya kuendelea na usajili, tafadhali soma na ukubali Kanuni Rasmi za Mashindano.
Usajili hauimaanishi timu imethibitishwa. Timu itakuwa rasmi baada ya malipo kamili kuthibitishwa na Kamati ya Pande Cup.
Usajili wa Pande Cup unafanyika 100% kupitia www.pandecup.co.tz. Hakuna usajili wa karatasi wala usajili wa timu uwanjani.
Timu itatakiwa kuweka jina la timu, taarifa za kocha/meneja, namba ya simu, eneo, wachezaji, nafasi za wachezaji, namba za jezi, picha za wachezaji, na picha ya kocha/meneja.
Muhimu: kujaza form hakumaanishi timu imethibitishwa. Baada ya kutuma taarifa, timu itakuwa katika hali ya Registration Received.
Malipo kamili ndiyo yanathibitisha nafasi ya timu kwenye mashindano.
Timu itathibitishwa rasmi baada ya malipo kamili ya ada ya ushiriki kuthibitishwa na Kamati ya Pande Cup.
Timu ambayo haijathibitishwa haitapangiwa kundi, haitapangiwa ratiba, na haitaruhusiwa kushiriki mechi.
Kamati haiwajibiki kutenga nafasi ya kundi, ratiba au ushiriki wa timu ambayo haijakamilisha malipo na kuthibitishwa rasmi.
Inapakua takwimu rasmi za uwanjani......